Mtoto mdogo aliyefahamika kwa jina la Jason Akwilo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita amefariki dunia baada ya kuzama kwenye kisima kilichopo eneo la vinyunguni mtaa wa Lumwago Mjini Mafinga.
Akithibitisha taarifa hiyo Mwenyekiti wa Mtaa huo Nausi Kalinga amesema alipokea taarifa kutoka kwa bakozi wake na baadaye akaenda eneo la tukio na kukuta mtoto huyo akiwa amezama kwenye kisima hicho ambapo alitoa taarifa kwa jeshi la zimamoto ambao walifika eneo la tukio na kuutoa mwili huo
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Upendo Michael Msite amesema katika Kata yake kumekuwa na matukio lukuki hivyo wameanzisha oparesheni ya kuhakikisha visima vyote vinakuwa na mifuniko ili kuepukana na majanga kama hayo.
Mwili wa mtoto huyo umepelekewa katika chumba Cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mji wa Mafinga.