MWENYE ULEMAVU WA MACHO ALIYEHITAJI MSAADA WA MAKAAZI, HATIMAE AJENGEWA NYUMA

Hassan Msellem
0

Agosti 18.2021 mwandishi wa habari hizi aliandika habari iliyomuhusu Mohammed Juma Ali mwenye umri wa miaka 45, ambaye pia ni baba wa watoto nane anayeishi kijiji cha Kidemeini Shehia ya Kwale Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba kuhusiana na msaada wa kupatiwa makaazi baada ya nyumba yake kuanguka kutokana na kukosa matunzo baada ya kupata ulemavu wa macho iliyotokana na tatizo la presha ya macho.


Saleh Hassan Hamad, ni msamaria mwema ambaye aliguswa na hali ngumu ya kijana Mohammed mwenye ulemavu wa macho na kuchukua hatua za kumjengea nyumba yenye vyumba viwili vya tofali pamoja na kuiyezeka kwa mabati ya kisasa ili kumpa faraja kijana huyo.

Alisema “Sio kwamba nina uwezo nzuri wa kifedha lakini kama mwanadamu ambaye Mwenyezi Mungu amenijaalia rizki kidgo niliguswa na hali ya huyu mwanadamu mwenzangu nikaona kuna haja ya kumsaidia hivi nyumba viwili ili aweze kujistiri na watoto wake maana hali ilikuwa mbaya sana ndugu mwandishi kama ulivyokuwa unaona”

Kwa upande wake baba huyo wa watoto nane mwenye ulemavu wa macho ametoa shukurani zilizoonekana kutoka kwenye uvungu wa moyo wake kwa mzee Saleh Hassan Saleh, anayeishi Bahanasa Wete ambaye alimpatia msaada huo wa kumjengea nyumba lakini licha ya kujengewa vyumba hivyo viwili amesema kuwa bado anakabiliwa na changamoto ya uhaba wa nyumba kutokana ukubwa wa familia yake.


“Kwakweli namshukuru san asana ten asana bwana Saleh Hassan Saleh kwa imani yake ambayo Allah amemjaalia kwa kunijengea nyumba hii ya tofali iliyoezekwa bati za kisasa yani bati nyekundu kwakweli ni kama siamini hivi kutokana na hali ngumu tuliokuwa nayo kulala chumba kimoja na mkeo na watoto wako sio jambo jepesi lakini licha ya shukurani hizo bado vyumba viwili ni kidogo sana kwasababu familia yangu ni kubwa kwahivyo watoto wa kike wanalala na wakiume na sio wadogo tena kwahivyo watu wenye uwezo waweze kunisaidia angalau nipate chumba kingine kimoja” alisema


Mariam Ali Haji, ni mke wa baba mwenye ulemavu wa macho alisema kutokana hali ya ulemavu aliyonao mume wake hali maisha kwao imekuwa ngumu sana kiasi kwamba baadhi ya siku inapita bila ya kuingiza chochote tumboni.

“Alhamudulliah tumepatiwa msaada wa kujengewa vyumba hivi viwili si haba kwa ali tuliokuwa nayo ila ndugu mwandishi hali yetu ya kimaisha ni mbaya mbaya mbaya mno kwasababu kama unavyomuona baba wa familia ndio huyo hapo kutokana na hali inamuiya vigumu sana kufanya kazi za kupata pesa maana kama unavyojua kuwa kazi huku ni ngumu sana mtu ende pwani, apige mkaa, alime ndipo apate chochote sasa na yeye kwa kazi sasa hivi haziwezi tena tuomba wasamaria wema watusaidie” alisema mama huyo

Bwana Mohammed, ana watoto nane ambapo sita kati ya hao wanaendelea na masomo ambapo mmoja kati yao ambaye ni mkubwa wakike ameacha kusoma akiwa darasa la sita kutokana na hali ngumu ya kimaisha.

"Nina watoto sita wanaosoma Skuli kwa Sasa na mmoja ambaye ni dada yao ameacha kusoma akiwa darasa la sita kutokana na Hali zetu ngumu za kimaisha maana alikuwa anaondoka nyumbani hajatia kitu tumboni na sina cha kumpa na anarudi hakuna chakula hivyo akaamua kuendelea na masomo na hao wanaendelea na masomo ndio hivyo hivyo siku wanakwenda siku hawaendi" alisema 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top