Mwalimu Aanika Barua ya Mapenzi Aliyoandikiwa na Mwanafunzi Wake wa Kiume

0

 Mwalimu wa shule ya sekondari ameshiriki barua ya mapenzi aliyopata kutoka kwa mwanafunzi wake wa kiume ambaye alidai kuwa mwalimu huyo mrembo ameteka moyo wake.

Mwanafunzi huyo alifungua moyo katika barua hiyo akisema kila anapomuona mwalimu huyo ambaye yuko kwenye mafunzo, ubongo wake huacha kufanya kazi.


Aliongeza kwamba hukosa ujasiri wa kumwendea mwalimu huyo na kumfungulia moyo wake na ndio maana aliamua kudhihirisha mapenzi yake kwake kupitia barua. Alifafanua zaidi kwamba uzuri wa mwalimu huyo humumaliza sana na kwamba japo bado yuko sekondari, ana mipango ya kuwa tajiri.

Barua hiyo ilisomeka; “Aunty Chioma, Hili linaweza kuonekana geni kwako lakini namaanisha kila neno. Tangu nilipokuona shuleni kwa mara ya kwanza, ilikuwa kana kwamba chembechembe za ubongo ziliacha kufanya kazi." "Kila nikikuona itakuwa kana kwamba moshi unanitoka machoni mwangu. Uzuri wako unaniua sana. Ingawa bado niko sekondari, nina mipango ya kuwa tajiri. Najua utasema mimi ni mvulana mdogo lakini ngoja nikuambie ukiwa kwenye mapenzi umri haujalishi. Ninakuwa bure sana kwa sababu ninaendelea kukufikiria.


"Kila nikifumba macho naona picha yako. Tafadhali zingatia ombi langu na unifanye kuwa muhimu kwa mara moja."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top