Mwalimu wa Sekondari Manispaa ya Mtwara Mikindani afutwa Kazi

0

 KIKAO cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara kimeazimia kumfukuza kazi mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi iliyopo Manispaa hiyo kwa kosa la utoro wa muda mrefu.

Akizungumza mei 26.2023  katika kikao hicho, Mstahiki Meya wa Manispaa ya hiyo, Shadida Ndile amesema baraza limeazimia kumfukuza kazi mwalimu wa shule hiyo, Prosper Nicholous kwa kosa hilo bila taarifa yoyote kwenye eneo lake la kazi.

‘’Baada ya kupitia sheria na kanuni zote za utovu wake wa nidhamu, basi baraza hili limeamua kwa pamoja limemfukuza kazi huyu mtumishi, mwalimu wa shule ya sekondari ya Mtwara ufundi kwa kosa ala utoro wa muda mrefu bila kuwepo kazini’’,amesema Ndile

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Kanali Emmanuel Mwaigobeko amesema mwalimu huyo hajaonekana kazini tangu Septemba 29, 2022 na hata pale alipoandikiwa barua na uongozi wa Manispaa hiyo ya kujieleza juu ya taarifa yake yoyote hakuweza kufanya hivyo badala yake alibaki tu kimya.

Aidha, kikao hicho kimejadili taarifa mbalimbali za Halmashauri kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top