Mwanafunzi ajiteka ili kuwatapeli wazazi wake

0

Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi shirikishi ( CUHAS) cha Bugando mkoani Mwanza amekamatwa na Jeshi la Polisi wakati alipojaribu kuwalaghai wazazi wake kuwa ametekwa na watekaji wanahitaji fedha ili waweze kumuachia.


Kwa mjibu wa kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema, mwanafunzi huyo alijiteka na kukaa gesti moja iliyopo Igongo katika chumba namba 103 kwa lengo la kujipatia kipato.

"Huyu alikuwa amepumzika kitandani miguu juu maisha yanaendelea na yeye alikuwa anaendelea kunywa bia zake, Polisi baada ya kumkamata tulimhoji na alikiri kuwadanganya wazazi na viongozi wa chuo kwamba alikuwa ametekwa ili apewe fedha aendelee kula starehe," amesema kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, amewahiza vijana kuacha janjajanja kwa kuwa wameaminiwa na familia zao kwa kuwalipia gharama kubwa katika vyuo kuvumilia na kusoma kwa bidii mpaka pale watakapo hitimu masomo, waende kutumia fedha zao wenyewe pindi watakapopata ajira.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top