Mwanamke nchini Kenya alizirai na kupoteza maisha akiabudu katika kanisa moja la eneo bunge la Lang'ata katika kaunti ya Nairobi Jumapili - Mei 15, 2023.
Awali, mwanamke huyo alidhaniwa kuzirai
tu na wahudumu wa kanisa wakaitwa kumsaidia, Lakini, hali yake ilivyozidi kuwa
mbaya, ilikuwa wazi kuwa matibabu ya dharura yalikuwa yanahitajika.
Alikimbizwa katika Hospitali ya Mbagathi
lakini madaktari wakabaini kuwa alikuwa amefariki hata kabla ya kufika katika
hospitali hiyo.
Kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Nairobi Adamson Bungei ameuthibitishia umma kuwa uchunguzi unaendelea kumtambua marehemu na chanzo cha kifo chake.
"Bado hatujabaini chanzo cha kifo chake
Upasuaji wa mwili umefanywa ili kutusaidia katika uchunguzi wetu
unaoendelea," Bungei alisema.