Mwanamke Mwingine atupa Kichanga chake Barabarani

0

 Mwili wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa wiki tatu umekutwa umetupwa kwenye njia ya mtaa wa Kileleni kata ya Kitangiri wilayani Ilemela mkoani Mwanza hali iliyozua sinfofahamu kwa wananchi wa eneo hilo.


Wakazi wa mtaa huo wamesema majira ya saa moja asubuhi wakati watoto wao wakienda shule waliona kichanga hicho ndipo wakawajulisha wazazi wao ambao walienda na kukiangalia na kukuta kichanga hicho tayari kimeshapoteza Maisha.

Bado haijafahamika mara moja ni nani ametupa mwili huo katika eneo hilo huku diwani wa kata ya kitangiri ulipo mtaa huo wa kileleni akisema baada ya taratibu za polisi kufanyika watalazimika kuuzika mwili wa kichanga hicho.

Stella Kilawe ni afisa mtendaji wa mtaa wa Kileleni amesema kitendo hicho cha kutupa kichanga siyo kizuri na kutoa ari kwa wakazi wa mtaa huo na mitaa Jirani kuacha tabia hiyo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top