Mwizi wa Bodaboda auawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuua mwenzake

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limethibitisha kuuawa kwa dereva Bodaboa aliyefahamika kwa majina ya Msuko Abrahama Juma (30) mkazi wa Mikindani, kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni na mkononi kisha mwili kutupwa porini.

Akizungumzia tukio hilo Mei 02, 2023 ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi Nicodemus Katembo, amesema mauaji hayo yamefanyika Aprili 24 mwaka huu, katika kijiji cha Mnyundo wilaya ya Mtwara, yakitekelezwa na mtuhumiwa Ahmad Said Kofi (25) mkazi wa Mikindani.

Kamanda huyo wa Polisi amesema mtuhumiwa huyo alimkodi marehemu kama abiria ili ampeleke kijiji cha Mnyundo ambako alitekeleza mauaji hayo.

Amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya tukio hilo aliondoka na Pikipiki aina ya TVS ambayo ni mali ya marehemu na kuipeleka kwa rafiki yake aitwaye Saidi mkazi wa kijiji cha Mnyundo, ambaye naye baada ya kusikia taarifa za kuuawa kwa mtu na kunyang’anywa Pikipiki, aliamua kuipeleka Pikipiki hiyo nyumbani kwa Mama mzazi wa mtuhumiwa.

Mama huyo naye aliambatana na mtoto wake wakike kwenda kichakani kuitelekeza pikipiki hiyo kabla ya wananchi kuiona na kutoa taarifa Polisi waliofika kichakani hapo kuichukua.

“Mtuhumiwa huyo alirudi Mikindani na ndipo taarifa za kurudi kwake Mikindani ziliwafikia wananchi na kuamua kumkamata.”

“Lakini kabla ya kumkamata mtuhumiwa huyo alianza kutimua mbio na ndipo wananchi walimfukuza hadi walipomkamata eneo la Mbae na kuanza kumshambulia kwa mawe na fimbo hadi kufariki dunia.” Ameeleza Kamanda Katembo.

Aidha amesema, miili ya marehemu wote wawili (Dereva Bodaboda na Mtuhumiwa wa mauaji) imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top