MZEE ALIYEMPA UJAUZITO BINTI WA MIAKA 13, KUPIMWA DNA.

Hassan Msellem
0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba kitengo cha upelelezi wa makosa ya udhalilishaji kimechukua hatua ya kumpima vinasaba (DNA) Mze e Hussein Abdalla Khamis anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 Mkaazi wa Shehia ya Kisiwani Wilaya Wete Mkoa wa Kaskazini anayetuhumiwa kumpa ujauzito binti mwenye umri wa miaka 13, anayesoma darasa la tano ambaye alijifungua tarehe 3 May, 2023 majira ya saa 7 mchana akiwa nyumbani kwao Kisiwani.

Lengo la kipimo hicho ni kuangalia usawa wa vinasaba baina mtoto na mzee huyo ili hatua nyengine za kisheria ziweze kufuatwa.


Kwa mujibu wa baba mtoto wa binti ambaye amepewa ujauzito na mzee huyo, amemuambia Mwandishi wa habari hizi kuwa licha ya Jeshi la Polisi kuamuru mzee huyo kufanyiwa vipimo vya DNA lakini amekiri kufanya tendo la ndoa binti huyo kwa mara kadhaa.


Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 4 mweiz Mei, 2023 majira ya saa 7 za mchana binti huyo alijifungua licha ya wazazi wake na walimu wa shule kutokugundua kuwa binti huyo alikuwa na ujauzito.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top