MZEE WA MIAKA 68 ATUHUMIWA KUMDHALILISHA MTOTO WA MIAKA MITANO NA KUKIMBIA.

Hassan Msellem
0

Mzee Azizi Hamad Hababu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 68 Mkaazi wa Kijiji Cha Mahuduthi Shehia ya Mkungu Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, ametoroka kusikojuilikana baada ya kutuhumiwa kumdhalilisha kingono mtoto mwenye umri miaka mitano Kwa kumtia vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vidole katika sehemu yake ya siri ya mbele na kumsababishia kutokwa na harufu mbaya.

Akisimulia jinsi alivyogundua Mtoto wake kuwa na Hali hiyo ya kutoa harufu mama mzazi wa mtoto huyo amesema wakati akiwa anamfanyia usafi Mtoto wake alihisi harufu Kali ambayo ilikuwa ikitoka sehemu za siri za Mtoto huyo ndipo alipochukua hatua za kumpeleka hospital kufanyia vipimo na kugundulika kuwa amekuwa na kawaida ya kuingizwa vitu sehemu yake ya uke.


"Kuna siku nilikuwa namuogesha nikawa nasikia harufu mbaya sana nikashituka ndipo nikamuhadithia mume wangu akaniambia basi tumpelekea hospital, ndipo tukampeleka hospital kumfanyia vipimo na tukaambiwa kuwa mtoto wenu kaingizwa vidole sehemu zake za siri za mbele, sasa tukawa tunamuuliza ni nani aliyekuwa anakufanyia ndipo akajibu ni Mzee Azizi" alisema mama wa mtoto huyo


Akikiri kutokea kwa tukio hilo Sheha wa shehia ya Mkungu Simai Faki Simai, amesema alipata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo kupitia ndugu wa Mzee Azizi Hamad Hababu ambao walifika kwake kutaka barua ya dhamana baada ya baadhi ya wanafamilia kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa.


Mwandishi wa Habari hizi alizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Abdalla Hussein Mussa, ili kufahamu hatua walizochukua kumtia mbaroni mtuhumiwa lakini kamanda huyo amesema bado hajapata taarifa za tukio hilo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top