Jeshi la polisi mkoani Mwanza limetangaza doria maalum ya kuwakamata na kuwaondoa katikati ya jiji hilo pamoja na kwenye vituo vya daladala vibaka wote wanaopora simu pamoja na wanaoshirikiana nao kuflash simu wanazoiba ili kuhakikisha wakazi wa jiji hilo wanaishi kwa amani.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ametembelea katika mitaa ya Rwagasore, Sahara na
Natta iliyopo katikati ya jiji hilo na ambayo inatajwa kuwa na vibaka hao
wanaopora watu simu na hela na kuwapa salamu kwa kutaka waache mara moja
vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
"Sasa nimetembea mimi mwenyewe makusudi kwa miguu na
napeleka ujumbe bahati nzuri nipo na maafisa hapa wanaosimamia askari kwa ajili
ya doria na askari wapo kwamba wafanye doria ya kutosha za kuhakikisha kwamba
wahalifu wote wanaojihusisha na wizi wa simu wanakamatwa na wanashughulikiwa
kwa nguvu zote kwa hiyo kuanzia leo natangaza kazi maalum ya kuhakikisha eneo
hili linakuwa salama kiasi kwamba hata mtu akisahau simu yake hapa chini
anaikuta natoa amelekezo ifanyike doria kali, ifanyike Misako mikali kero ya
wizi was imu iishe eneo hili"
Kwa upande wake mmoja wa wakazi wa jiji la Mwanza amepongeza hatua hiyo ya jeshi la polisi na kusema waliwahi kuwaripoti polisi vijana ambao walikuwa wanaishi chini ya karavati na kujihusisha na vitendo vya wizi.
"kulikuwa na karavati kulikuwa na watu wametengeneza kama
makazi lakini kwa kushirikiana na jeshi la polisi kituo cha pamba tulitoa
taarifa lilikuja difenda likawachukua wote na mpaka sasa tunaishi salama
kabisa"
Katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa amesema wameyakamata
magari Matano ya kubeba abiria ambayo madereva na makondakta wake wamekuwa
wakiyatumia kwa ajili ya uhalifu huku wakitumia majina ya manuari pindi
wanapotenda uhalifu huo