'PPC' YAADHIMISHA MIAKA 30 YA UHURU WA HABARI DUNIANI, AJENDA KUU-MAPAMBANO DHIDI YA GBV NA KULIPA KODI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI.

Hassan Msellem
0

 Na, Hassan Msellem, Idawaonline.com


Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kuongeza bidii ya kuandika habari dhidi ya janga la ukatili wa kijinisi na udhalilishaji ili kuisaidia jamii dhidi ya janga hilo.


Kauli hiyo imetolewa na afisa mdhamini Wizara ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Pemba Hafidh Ali Mohammed, katika maadhimisho ya miaka 30 ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyoandaliwa la klabu ya waandishi wa habari Kisiwani PPC huko Mjini Chake Chake, amesema kutokana kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji waandishi wa habari nchini wanapaswa kuongeza juhudi za kuandika habari na Makala mbali mbali kuhusu ili kuishinikiza Serikali kuchukua juhudi za ziada katika kukabiliana janga hilo.


Alisema “Niwasihi sana ndugu zangu wanahabari katika kuongeza juhudi za kuandika habari ambayo zinatoa elimu kwa wananchi dhidi ya kujikinga na matendo ya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji pamoja na kuishinikiza Serikali kuongeza juhudi kuhakikisha inakabilina na matendo hayo”


Aidha amesema, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi, anathamini mchango wa wanahabari na vyombo vya habari kama ni muhimili muhimu wa kuikumbusha Serikali katika jukumu lake la kuwatumikia wananchi sambamba na utoaji wa taarifa mbali mbali za Serikali.

Afisa mdhamini Wizara ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Pemba Hafidh Ali Mohammed.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC) Bakar Mussa Juma, amesema Klabu ya waandishi wa habari Pemba ni miongoni mwa klabu 10 bora kati ya klabu 28 Tanzania ambayo inatimiza wajibu wake kutoa taarifa na elimu kwa jamii.


“Pemba Press Club ni moja ya klabu bora Tanzania ambayo inatambulika katika umoja huo hata na wafadhili wetu ikiwemo Ubalozi wa Sweeden katika shirika lake la Msaada la SIDA” alisema  

Katibu wa Klabu hiyo Ali Mbarouk Omar, amesema ushirikiano baina ya Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ni miongoni mwa hatua za maendeleo zilizofanywa na klabu hiyo kwani itachochea waandishi wa habari kutapa taaluma ya kulipa kodi kwa njia za kisasa za kielektroniki sambamba na kutoa taaluma hiyo kwa wananchi.


Akiwasilisha mada juu ya mfumo wa ukusanyaji kodi kwa njia za Kielekroniki kwa waandishi wa habari, Afisa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Khairat Said Soud, Amesema miongoni mwa wajibu wa waandishi wa habari katika ukusanyaji wa kodi ni kuelimisha jamii kuhusu kodi na umuhimu wake kwa maendeleo taifa.

Alisema “Nyinyi ni muhimili muhimu sana katika taifa kwasababu munao uwezo wakuifikia moja kwa moja kupitia vyombo vyenu vya habari hivyo basi baada ya kuwapatia mafunzo haya ulipaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki mukayatowe mafunzo kwa wananchi ili waweze kufahamu haki na wajibu wao wa kulipa kodi na kudai risiti”

Sambamba na hilo amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili kupitia mfumo huo ni pamoja wafanyabishara wengi kutokufanya usajili na kupelekea uvujaji wa mapato.

“kwakweli bado mfumo huu wa kielektroniki unakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo wafanyabishara kutokutoa risiti na wananchi kutokuwa na muamko wa kudai risiti, kutokuonana baina ya mifumo ya kukusanya kodi na mifumo ya wafanyabiashara, kupotea kwa kumbukumbu za mauzo, kutoa taarifa za mauzo zenye viwango vya chini pamoja na kuwa na njia tofauti za kutolea risiti kwa wafanyabiashara” afisa Tehema ZRA

Maadhimisho ya miaka 30 ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwa upande Klabu ya Waandishi wa Habari Pemba (PPC) yamefadhiliwa na Umoja wa vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) pamoja na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).


Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani huadhimishwa Mei 03 kila mwaka na kuwa na kauli mbiu ambapo kauli mbiu yam waka huu inasema “KUUNDA MUSTAKABALI WA HAKI UHURU KUJIELEZA KAMA KICHOCHEO CHA HAKI NYINGINE ZOTE ZA BINADAMU”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top