Rais Samia afanya uteuzi wakuu wa Mikoa!

0

 Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya baadhi ya wakuu wa mikoa, uteuzi wa mkuu wa mkoa, uhamisho wa wakuu wa mikoa na uteuzi wa mkuu wa wilaya.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Said Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, akichukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Queen Sendinga aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, amehamishiwa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akichukua nafasi ya Makongoro Nyerere aliyehamishiwa Rukwa.

Pia amemteua Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo, akichukua nafasi ya Mtanda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Taarifa imeongeza kuwa uhamisho na uteuzi huo unaanza mara moja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top