Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan mei 15 2023 amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:
1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu inesema Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.