Rais Samia : Serikali itaendelea kuboresha uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini

0

 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha vyombo vya habari na utangazaji unakua na teknolojia  za juu za habari zinazozingatia mila na desturi.

Haya ameyasema  jijini Dar es Salaam wakati akizindua  Mradi wa Minara ya Kurusha Matangazo ya Television Ardhini (DTT), na kueleza kuwa hivi sasa tasnia ya habari imekua na muelekeo mzuri wa maazimio na hii inatokana na uhusiano uliopo baina ya vyombo vya habari na vyombo binafsi.

Aidha Rais Samia ameviagiza vyombo vya habari kuhakikisa maudhui yote yanayotolewa yanafuata mila na desturi za Tanzania na kuiagiza Wizara ya Habari kuhakikisha inatekeleza yale yote yanayokwamisha vyombo vya habari na kuwa marekebisho ya sheria na kanuni  ya vyombo vya habari yatakapotoka ihakikishe haitakua tena na malalamiko .

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mradi huo utangeza wigo na kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kupata habari, matukio na burudani za ndani na nje ya nchi kwa ubora na viwango vya kimataifa.

Vilevile ameweka wazi kuwa sekta ya habari imeendelea kukua na vyombo vimeongezeka sana kwa sasa kuna ongezeko la vituo Vya kurusha matangazo ya redio kutoka 210 mwaka 2022 hadi 218 April 2023 huku vituo vya televisheni vikiongezeka kutoka 56 mwaka 2022 hadi 68 April 2023

kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media LTD Tido Mhando, amebainisha kuwa mradi huo umegharimu shilingi bilioni 50 na utasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya televisheni huku akieleza changamoto zilizopo kwenye vyombo vya habari.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top