Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt.Fatma Mganga Amewataka Walimu Wakuu,Maafisa Elimu wa Kata na Wilaya Zote za Mkoa Huo Kutimiza Majukumu yao Ipasavyo ili Kuinua Kiwango cha Ufaulu wa Wanafunzi Mkoani Humo.
Akizungumza Katika Kikao Kazi Baina yake na Viongozi hao Dkt. Mganga Amesema Hali ya Elimu Mkoani Singida Hairidhishi ikilinganishwa na Maeneo Mengine Nchini Huku Akiwahimiza Kufanya Tathmini katika Shule zao na Kuandaa Mikakati itakayosaidia kuondokana na Hali hiyo.
Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Bahi Boniphace Wilson Ambaye Alialikwa Kutoa Uzoefu wa Namna Wilaya Hiyo Ilivyopiga Hatua Katika Elimu Kulinganisha na Miaka Nyuma Ambapo ilikuwa Duni Kielimu Ameeleza Mikakati Ambayo imewasaidia Kupata Ufanisi.
Mratibu wa Program ya Shule Bora Mkoani Singida Samwel Daniel Amesema Ili kupata Ufanisi katika Kuinua kiwango Cha Elimu Singida Ufuatiliaji wa Karibu kutokana kwa Viongozi Unapaswa Kuongezeka Sambamba na Uwepo wa Ripoti katika Utekelezaji wa Mikakati inayopitishwa katika Vikao.
credit-Wasafifm