Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe limewataka maofisa na askari wake kuhakikisha kuwa wanazingatia misingi ya maadili mema katika utendaji kazi.
Hayo yamesemwa Mei 24,2023 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi wa Polisi ACP John Makuri wakati kikao kazi Cha kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe ACP Hamis s Issah.
Kamanda Makuri, amesema ukifuata taratibu na miongozo iliyopo katika Kazi zetu itasaidia kupunguza malalamiko kwa Wananchi kwani Jeshi la Polisi Tanzania lina Imani na watendaji wake pia amesisitiza kuwa lazima uhalifu udhibitiwe na usifichwe.
Amewataka maofisa na askari kuwa na usimamizi mzuri wa ndani kuachana vitendo ambavyo ni kinyume na utaratibu wetu mfano rushwa ambayo matokeo yake unaweza kupoteza kazi au hata kufikishwa mahakamani tusipokuwa makini.
Vilevile amewahasa kuwa na mawasiliano mazuri lakini pia amesisitiza askari wote kuwa na upendo na kushauriana na kusaidiana ili tuweze kuwa pamoja
Akizungumza wakati wa kikao hicho Kamanda anayeondoka Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Hamis Issah amewataka Askari kuendelee kupambana na uhalifu ili mkoa huo uendelee kuwa salama lakini pia kumpa ushirikiano mzuri Kamanda mpya.