Serikali kuleta mfumo wa kutabiri Mafuriko

0

 Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2023/2024 ambapo amesema Wizara ya Maji inaendelea na maandalizi ya mfumo wa utabiri na kutoa taarifa za awali za kutokea kwa majanga ikiwemo mfumo wa utabiri wa mafuriko na tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa.


Waziri Aweso amesema; “Wizara inaendelea na maandalizi ya mfumo wa utabiri na kutoa taarifa za awali za kutokea kwa majanga kupitia Mradi wa Operational Decision Support System (ODSS) through Enhanced Hydro-Meteorological Services.”

“Mfumo huo wa Kielektroniki unahusisha mifumo ya utoaji wa taarifa za rasilimali za maji (Water Resources Management Information System), ugawaji wa maji (Water Use Permit Analysis Tool), mfumo wa utabiri wa mafuriko na tahadhari (Flood Forecasting and Early Warning System), utabiri wa misimu ya maji katika vyanzo vya maji (Seasonal and Flow Prediction Tool) na kusaidia uendeshaji wa mabwawa ya maji (Dam Operational Support Tool).

“Hadi Mwezi Aprili 2023, Wizara imetoa mafunzo yanayohusu mfumo huo kwa Wataalamu wa Bodi za Maji za Mabonde yote tisa, Idara ya Rasilimali za Maji na Kitengo cha TEHAMA cha Wizara.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top