Serikali wilayani Makete yaanza ujenzi madarasa ya Mfano Kinyika

0

Serikali imetoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 69,100,000 kupitia mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba viwili vya mfano Madarasa ya Awali ambapo tayari ujenzi umeanza upo katika hatua ya Msingi.



Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amekagua ujenzi huo na kumsihi mkandarasi mzawa Ndg. Onesta Sanga ambapo amemtaka kukamilisha majenego hayo kabla ya mwezi wa saba mwaka huu.

Mhandisi wa Ujenzi Halmashauri ya Wilaya ya Makete Emily Maganga amesema fedha hizo zitajenga madarasa mawili ya mfano na ukuta kuzunguka madarasa, vyoo matundu 6 kati ya hivyo ni vyoo vinne vya watu wenye mahitaji maalumu na vyoo viwili vya kawaida.
 Juma Sweda amekutana Pia na Wenyeviti wa Vitongoji na Serikali za Vijiji Kata ya Kinyika kuzungumza masuala mbalimbali ya Kimaendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi ya Barabara, Elimu, Afya n.k

Mhe. Sweda amepokea changamoto ya Barabara ya Kinyika, Mwambwalo-Kikondo ambapo kwa sasa Barabara hiyo imefunga haipitiki na kuwaagiza TARURA kuleta mitambo haraka iwezekanavyo kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo aambayo Serikali ilishatenga fedha.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwambwalo Kijiji cha Kinyika Aloyce Sanga amesema uchumi wa Wananchi wa Kitongoji hicho na Bonde la Matamba umeporomoka kwa sababu ya ubovu wa Barabara kwa kuwa wananchi wa Kata ya Kinyika, Matamba na maeneo jirani wengi wao wanajishughulisha na Kilimo cha Viazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top