Spika Tulia: Simuogopi Sugu! Nimefanya kazi kubwa mbeya

0

 Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema ahofii kukabiliana na aliyewahi kuwa Mbunge Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ endapo watakutana katika kinya’ng’iro cha kugombea jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao 2025 utakaokuwa huru na haki.


Dk Tulia ametoa msimamo huoMei 4, 2023 wakati akijibu swali katika mahojiano maalumu na Wasafi fm yaliyofanyika katika makazi rasmi ya Spika Jijini Dodoma.

Pamoja na mambo mengine, Spika aliuzwa ikiwa hatishiki kukabiliana na Sugu’ katika uchaguzi unaoitwa huru na haki, hasa ikizingatiwa kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, wapinzani wengi waliamini kuna nguvu ya ziada ya dola ilitumika kuwabeba walioshinda. Also Read

Pikipiki yalipuka na kuteketea jijini Mwanza Kitaifa 41 min ago Pikipiki yalipuka na kuteketea jijini Mwanza Kitaifa 41 min ago

“Sihofii kupambana naye, niko vizuri sina wasiwasi na hilo naomba Mungu aniweke, nimefanya kazi kubwa, nyie nendeni Mbeya Mjini mtaamini,’ amejinasibu Dk Tulia.

Na akaongeza kusema: “Hata yeye anajua (Sugu), hao wanaojadili mtandaoni nadhani hawajafika Mbeya wala hawapajui wala kuwasikia Mbeya, sasa nyie (waandishi) mnakaribishwa halafu mtawanyike na mkaulize hapa Mbeya Mjini mbunge ni nani, mtapata majibu.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top