TAASISI YA ‘ZYCO’ YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA, AJENDA KUU, MFUMO MPYA WA MABADILIKO YA TAASISI

Hassan Msellem
0

 Na, Hassan Msellem, Idawaonline.com Pemba

Taasisi ya Zanzibar Youth Care Organization (ZAYCO) jana Mei 20.2023 imefanya mkutano mkuu wa huku ajenda kuu ikiwa ni mabadiliko ya mfumo mpya ya taasisi hiyo katika idara zote ikiwemo wafanyakazi wa taasisi hiyo pamoja viongozi wake.

Akiwasilisha Sera ya Utumishi na Mabadiliko ya Vifungu vya Katiba katika mkutano mkuu wa mwaka wa taasisi hiyo huko katika ukumbi wa ofisi za Wilaya Mkoani Pemba, Afisa Mbadilishaji Tabia Kijamii wa taasisi hiyo Abdalla Saleh Issa, amesema taasisi hiyo imeamua kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa shughuli zake ikiwemo kuondosha mfumo wa uanachama na badala yake kuwa wafanyakazi kwa njia ya kufanya maombi.

 

“Miongoni mwa mambo ambayo sera hii imeangazia ni pamoja na suala la uana chama yani badala ya kuwa na wanachama kwa mfumo wa kujaza fomu au kupendekezwa badala yake tutakuwa na mfumo wa wafanyakazi ambao watafanya maombi kwa mujibu wa nafasi wanazotaka kutumikia ili kuongeza ushindani katika taasisi” alisema


Akieleza mabadiliko ya baadhi ya vifungu katika Katiba ya taasisi hiyo, amesema ni mabadaliko ya kupatikana kwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo ambapo kwa mujibu wa katiba ya hivi sasa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo hupatikana kwa mfumo wa uchaguzi ambapo kupitia Sera hiyo Mkurugenzi atapatikana kupitia mfumo wa maombi kama zilivyo nafasi nyengine.


“Suala la upatikanaji wa Mkurugenzi pia nalo ni miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye Sera hii kwa maana kwamba kwa sasa Mkurugenzi wa taasisi anapatikana kwa kupigiwa kura na wanachama lakini endapo rasimu hii itapitishwa nafasi ya Mkurugenzi itatakiwa kuombwa ili kuongeza unafisi wa taasisi na hisia mkanganyiko katika taasisi” alisema

Afisa Mbadilishaji Tabia Kijamii wa taasisi hiyo Abdalla Saleh Issa.

Akitoa maoni juu ya Sera hiyo mwanachama wa taasisi hiyo Haji Khamis Mossi, amesema kuondoshwa kwa mfumo wa uchaguzi katika kuwapata viongozi wa taasisi hiyo ni kunyima haki ya uhuru wa kuchagua kwa wanachama wa taasisi hiyo


“Binafsi sikubaliani na Sera ya kufanya maombi katika nafasi za uongozi katika taasisi kwasababu mfumo wa maombi utanyima haki ya na uhuru wa wanachama kuchagua kiongozi wanaempenda hivyo nashauri viongozi wa taasisi akiwemo Mkurugenzi waendelee kupigiwa kura kama ilivyo hivi sasa” alishauri

Mwanachama wa taasisi hiyo Haji Khamis Mossi.


Akizungumza na wanachama pamoja na viongozi wa taasisi hiyo katika mkutano mkuu wa mwaka wa taasisi hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkoani     Katibu Tawala Wilaya ya Mkoani Bi. Miza Hassan Faki, amesema vijana wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa ajira hivyo ameitaka taasisi hiyo kuwashirikisha zaidi vijana katika miradi wanayoifanya ili waweze kuondokana na changamoto zinazowakabili.


Aidha amewataka vijana kuwa umoja na mshikamano katika kuendeleza vikundi vya ujasiriamali ili lengo la kuanzishwa kwa miradi hiyo liweze kufikiwa.

Katibu Tawala Wilaya ya Mkoani Bi. Miza Hassan Faki.


Kwa upande wake afisa Uhamasishaji na Uwezweshaji vijana Kiuchumi kutoka idara ya Vijana Pemba Seif Edward Kabeyo, amesema hatua za maendeleo ambazo zimefanywa na taasisi hiyo katika kuwasaidia vijana kiuchumi zinaridhisha ikilinganishwa na taaisi nyingi kisiwani Pemba.


Akiwasilisha ripoti ya fedha ya mwaka 2021 hadi Mei 2023 afisa fedha wa taasisi hiyo Abdul-karem Yusuf Ayoub, amesema hadi kufikia mwezi April mwaka huu taasisi hiyo imefanikiwa kupata ruzuku ya shilingi milioni kumi na tatu laki nane na sitini elfu mia tatu na ishirini ili kuendeshea miradi mbali mbali ikiwemo mradi wa afya ya mama mzazi na mtoto.

 

Nae afisa mipango wa taasisi ya ZYCO Abrahman Kassim Juma, amesema taasisi hiyo imedhamiria kutoa elimu juu ya shughuli mbali mbali za maendeleo kwa vijana ikiwemo shughuli za Kilimo, ufugaji na viwanda.


Afisa ufuatiliaji na tathmini wa taasisi ya ZYCO Ridhawan Haji Pandu, amesema miradi ambayo inaendeshwa na taasisi hiyo vijana wengi wamefanikiwa kuinuka kiuchumi hususan katika sekta ya kilimo na ufugaji. 


Katika Mkutano mkuu wa mwaka wanachama wa Taasisi hiyo wamepata fursa ya kuthibitisha wajumbe wa bodi ya wadhamini wa taasisi.


Taasisi ya Zanzibar Youth Care Organization (ZYCO) imeanzishwa rasmi mwezi february 2018 ikiwa malengo ya kuwawezesha vijana kiuchumi kuwa na afya salama, kuwa viongozi bora wa baadae na kupinga vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top