Ugomvi wawaponza fisi, wachomwa moto na wananchi

0

  Wananchi wenye hasira kali wa Mtaa wa Mbae chundi wamewapiga na kuwachoma moto fisi wawili waliokutwa ndani ya shimo la kisima wakipigana na kushindwa kutoka huku wakipiga kelele.

Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa serikali Mtaa wa Mbae Chundi, Sada Ally alisema kuwa chui wamekuwa tishio katika eneo hilo na kusababisha wananchi wengi kuogopa kufuga mifugo mbalimbali.

“Hawa fisi wamekuwa wakituathiri sana yaani usiku wa kuamkia jana walikuja nyumbani kwangu mabandani nikawafukuza yaani hatuna raha wanakula mifugo yetu sana yaani wanaonekana hadi asubuhi,” amesema.

“”Siku moja siku moja mama mmoja alikuwa anatoka feri asubuhi akakutana na fisi yaani wamekuwa wakutembea na kufanya fujo hivyo tunawahofia usalama wetu na familia zetu kama zipo mamlaka zije zitusaidie maana kwa sasa wanatembea hovyohovyo,” amesema.
Naye Salum Mussa mkazi wa Mtaa wa Mbae Chundi alisema kuwa mwezi huu chui wamengezeka hali ambayo imeongeza hofu kwa usalama wa watu na mifugo.

“Tulipewa taarifa na mwenye eneo kuhusu fisi hao, tukaja kuwaangalia wako wawili. Tulipofika tulikuta tayari wananchi wenye hasira wameshachoma moto na kuwaua,” amesema.

Masoud Mohamed ambaye ni mkazi wa Mbae chundi, amesema kuwa fisi hao walikuwa wakipigana na kulia kwa sauti kubwa.
“Majirani wanaoishi hapa wanasema kuwa fisi hao walifika eneo hilo lakini walikuwa wanapigana mwishoni wakaangukia ndani ya kisima,” amesema Mohamed.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top