Vijana wadaiwa kuuawa kichawi mkoani Njombe

0

Wakazi wa kijiji cha Nkwimbili kilichopo kata ya Lupingu Wilaya Ludewa Mkoani Njombe wamekumbwa na wimbi la matukio ya vijana kuuliwa kwa njia ya kichawi ambapo vijana huugua kwa masaa machache kisha kupoteza maisha.


Wakitoa ya moyoni mbele ya jeshi la polisi la wilaya ya Ludewa ambao walifika kijijini hapo kwa lengo la kutoa elimu juu ya kupinga vitendo vya ukatili baada ya hivi jaribuni kutokea tukio la vijana kuwapiga baadhi ya wazee waliokuwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo vya kichawi.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo jeshi la Polisi wilayani humo liliwakamata vijana wote waliohusika sambamba na wazee hao waliotuhumiwa huku miongoni mwa wazee hao akiwemo bibi ambaye ndiye amekuwa akiwataja wachawi hao ambaye Wananchi hao humuita kwa jina la mpelelezi wao.

Wananchi hao wamezipigia magoti Mamlaka mbalimbali za sheria kuwaomba kuwaachia huru vijana pamoja na mpelelezi huyo ambapo jeshi la Polisi limewata kufuata sheria na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top