Viongozi wa Mkoa wa Njombe wamtembelea DC Makete baada ya Kupata Ajali ya Gari

0

Mkuu wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe Mhe.  Juma Sweda anaendelea vizuri na matibabu  katika Taasisi ya Mifupa Jijini (MOI) jijini Dar Es Salaam ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari ni miongoni mwa viongozi waliomtembelea Mei 25, 2023 kumjulia hali ambapo bado anaendelea na matibabu.

Mwingine aliyemtembelea hospitalini hapo kumjulia hali ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe na Mganga Mkuu Wilaya ya Makete Ligobert Kalisa


Mhe. Sweda alipata ajali ya gari Mei 22, 2023 barabara ya Matamba - Chimala eneo lenye kona nyingi akiwa ziarani kuelekea kata ya Mfumbi kwenye ziara ya kuzungumza na Viongozi wa Vijiji na Wananchi wa Kata hiyo.

Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omari (Kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe na Mganga mkuu wa wilaya ya Makete Dr. Ligobert Kalisa (Kulia) wakimjulia hali Mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda anayeendelea na matibabu katika taasisi ya mifupa (MOI) baada ya kupata ajali ya gari.

Taarifa hii ni Kwa mujibu wa Kitengo cha Habari wilayani Makete,IDAWA MEDIA,Tunakuombea Afya Njema Mkuu wa wilaya ya Makete Mh.Juma Sweda na Mwenyezi Mungu akufanyie uponyaji. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top