Wakati wanafunzi kidato cha sita wakiendelea na mitihani yao ya kuhitimu elimu yao wamewaomba wazazi kuwatafutia fursa za kazi za kufanya ili kujiingizia kipato kuliko kurejea na kukaa bila kazi hali inayoweza kuhatarisha kesho yao.
Kauli hiyo imetolewa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Lupalilo iliyopo wilayani Makete Mkoani Njombe katika Mahojiano na Mtandao huu,ambapo wamesema kutokana na changamoto ya ajira wangetamani wazazi wawape mitaji au kuwatafutia fursa za kujiingizia kipato.
TAZAMA FULL VIDEO HII HAPA!