Wananchi Geita wadaiwa kuwapigia simu Zimamoto ili kuwasalimia Askari

0

 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewaonya baadhi ya wananchi mkoani humo wanaoipiga namba ya dharura ya 114 kwa ajili ya kuwasalimia askari kama mchezo na kuwataka kuitumia namba hiyo pale wanapokuwa wanahitaji msaada wa uokozi pamoja na majanga mengine.


Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoani humo Hamisi Dawa, amewataka wananchi hao kama wanataka kuwasalimia askari basi wafike kituoni hapo ili pia waweze kupata elimu sahihi ya matumizi ya namba hiyo.

"Tunawasihi wananchi wasitumie namba hii kupiga kwa ajili ya kusalimia au kutoa maneno yasiyofaa, waache michezo hiyo, sisi tukikubaini tutakuchukulia hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

"Unaweza kupiga simu kwa ajili ya kusalimi kumbe kuna mtu mwingine anapiga simu qmepata tatizo, hivyo laini itaonekana inatumika halafu unamnyima fursa mwenye tatizo kumbe amekumbwa na maafa.

"Niwasihi mtumie namba hii kutoa taarifa za majanga si kusalimia. Pia mnaweza kutumia namba za polisi kwani na wao tunashirikiana watatupa taarifa. Kama unataka kusalimiana pita kwenye kituo cha Zimamoto na Uokoaji tutasalimiana na kukupa elimu ya Zimamoto na Uokoaji katika maeneo yote mpaka nyumbani," amesema Afande Dawa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top