Watoto wachunwa ngozi na kukatwa ulimi Tabora serikali yatoa Tamko!

0

 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema baada ya kufuatilia wamebaini kuna ukweli juu ya taarifa za miili ya Watoto njiti mapacha waliofariki Kituo cha Afya Kaliua kukabidhiwa kwa Wazazi huku Watoto wakiwa wameng’olewa macho, kukatwa ulimi na kuchunwa ngozi kwenye paji la uso.


Waziri Ummy amesema “Tumelifuatilia suala hili, kuna ukweli, Uongozi wa Wilaya ya Kaliua umeshaanza kuchukua hatua, baadhi ya Watumishi wa Afya waliomuhudumia Mama huyu wameshasimamishwa kazi, nakemea vikali kitendo hiki, ninamuagiza RMO Tabora kusimamia vyema Weledi, Maadili na Miiko ya Watumishi wa afya”

Sakata hilo limeibuliwa na Mzazi wa Watoto hao Kisaka Mtoisenga Mkazi wa Ushikola, Kaliua Tabora kupitia kwa Mwanamtandao maarufu na Mdau wa masuala ya Kijamii Malisa @malisa_gj ambaye aliweka malalamiko ya Mzazi huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mzazi huyo amesema baada ya kupewa miili ya Watoto Watumishi wa Afya waliwaambia wakazike haraka kwakuwa Watoto njiti hawafanyiwi msiba na walipofungua box na kubaini miili imenyofolewa macho Watumishi hao wa Kituo cha Afya waliwajibu wakazike tu maana huo ni ushirika na hata walipoenda Polisi na kwa DC wa Kaliua waliambiwa wakazike tu kwakuwa ni ushirikina.
Chanzo: Millardayo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top