Wavuvi watatu wafariki baada ya mtumbwi kuzama majini

0

Watu watatu ambao ni wavuvi na wakazi wa kijiji cha Nungwe Kata ya Nyamilolelwa wilayani Geita wamefariki baada ya mtumbwi wao waliokuwa wanautumia kuzama majini na kupelekewa vifo vyao.


Akizungumza tukio hilo baada ya shughuli za uokoaji, Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uoakoji wilaya ya Geita, Wambura Fidel amesema kwenye mtumbwi huo kulikuwa wavuvi sita, kati yao wameokolewa watatu.

Amewataja manusura wa ajali waliookolewa ni Kurwa Thomasi (30), Dicksoni Alphonce ( 47) na Dickson Majura ( 22).

Aidha Mkuu wa wilaya ya Geita Corlnery Magembe amefika kuwapa pole wafiwa ambapo pia amewasihi wote wanaojihusiha na uvuvi wilayani Geita kuhakikisha wanazingatia taratibu za usalama majini na kuchukua tahadhari.

"Kwenye gari tunavaa mikanda ila kwenye maji tunavaa maboya, tusiache kuvaa maboya iwe unaenda umbali mrefu au mfupi au unajua unajua kuogelea au hujui" Ameelekeza Mkuu wilaya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top