Wazazi pokeeni ushauri kutoka kwa watoto wenu

0

Mkuu wa Kituo cha Polisi Morogoro Mrakibu wa Polisi (SP) Janeth Bernad Mei 24, 2023 amezungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Holycross iliyopo Manispaa ya Morogoro ambao ni wanaklabu ya Polisi katika kituo Kikuu cha Polisi walipofanya ziara kwa ajili ya kujifunza zaidi masuala ya ukatili wa kijinsia na watoto.

SP Janeth amewaeleza wanafunzi maana ya ukatili wa kijinsia na mbinu za kukabiliana nao ambazo ni pamoja na kukataa kulala na wageni, kukataa kushikwa sehemu za siri, kukataa zawadi kwa watu wasio wafahamu pamoja na kukataa kuitwa majina ambayo yanaviashiria vya kutaka kufanya ukatili kama vile mchumba, baby na mengineyo.

Aidha SP Janetha aliwataka wanafunzi hao kuwa wajasiri na kutoa taarifa kwa mzazi, mlezi, mwalimu au Polisi pale inapobidi ikiwa kuna mtu mwenye dalili ya kutaka kukufanyia ukatili pamoja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top