Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba Wafanyabiashara wa Kariakoo kusitisha mgomo na kufungua maduka yao huku akiagiza TRA kuacha kuwaonea Wafanyabiashara.
Akiongea na Wafanyabiashara wa Kariakoo , PM Majaliwa amesema “Nimeacha Bunge nimewafuata kuja kujua kuna nini!? Soko la Kariakoo tunalitegemea kutuingizia mapato ni lazima tulitulinze , nimesoma mabango yenu moja baada ya moja, kuna linalosema “TRA mmefukuza Wageni’ , mmeongelea EFD n.k, hakuna jambo mtalifanya tutalichukulia rahisirahisi”
“Tabia ya kuonea Wafanyabiasha ikome mara moja, hii ya kukusanya tu mnakusanya tu mpaka damu itoke hii sio sawa, wengine mnawazidishia kodi ili mkae nao chini muwaombe rushwa na hii rushwa inafanya Wafanyabiashara watoe hadi pesa zao za mauzo”
“Wafanyabiashara sikieni ombi la Serikali fungueni maduka yenu na matatizo yote keshokutwa tunayajadili keshokutwa, ningeweza kusema kesho lakini Mh.Rais amenituma kumwakilisha kwenye maziko ya Mh. Membe acha niende kesho asubuhi, ilitakiwa niende leo nimeghairi naenda asubuhi kesho nazika narudi tutatue matatizo”
Waziri Mkuu ameshangazwa na wanaodharau kauli za Viongozi Wakuu wa Kitaifa “Akitokea Mtu anasema lazima ulete barua ya agizo lililotolewa na Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, mtuletee huyo Mtu, Rais,Makamu wa Rais na Waziri Mkuu hawaandiki barua, wataandika barua ngapi?”
“Rais na Makamu wa Rais wanapoagiza sisi wa chini tunatekeleza, leo TRA Rais amesema kodi za miaka mitano mziache, nyie mnadai barua kwa Watu wa Kariakoo hivi Mfanyabiashara wa Kariakoo atapata wapi barua ya Rais? halafu unamwambia Mfanyabiashara hilo ni agizo tu la kisiasa, yaani agizo lililotolewa na Rais unasema ni la kisiasa hiyo ni dharau na natamani ningemjua aliyesema hivyo tumchukulie hatua”