Waziri wa Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda Nchini Uganda Charles Okello, ameuawa May 02, 2023 baada ya kupigwa risasi na mlizi wake ambapo Spika wa Bunge la Uganda Anitha Among amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Bungeni.
Inaripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka Nyumbani
kwenda kazini ambapo ghafla mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga
risasi juu huku akikimbiakimbia mtaani, majirani walisema walimsikia mlinzi huyo
akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi kwa muda mrefu
na Waziri huyo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa hii vinasema mlinzi huyo baadaye aliingia saluni moja iliyopo jirani na nyumba ya Waziri huyo kisha akiwataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki pia.