Ajira mpya za ualimu na kada ya Afya 2023

0

Serikali imesema zaidi ya watu 171,916 waliomba kazi ya ualimu na kada ya afya katika ajira zilizotangazwa na serikali mapema mwakaa huu 2023.

Katika taarifa iliyotolewa kwa Umma na Mhe. Angellah Kairuki Waziri wa Nchi, OR- TAMISEMI 05.06.2023 amesema 'Mtakumbuka kuwa mwezi Aprili, 2023; Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya'

Baada ya kupata kibali cha ajira, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilitoa tangazo kwa wahitimu mbalimbali wa Ualimu na Kada za Afya kuwasilisha maombi ya kazi kupitia mfumo wa kielektroniki wa kupokea na kuchakata maombi ya ajira kuanzia tarehe 12/04/2023 hadi 25/04/2023. 

Jumla ya maombi 171,916 yakiwemo ya Wanawake 76,190 na Wanaume 95,726 yalipokelewa kwenye mfumo, ambapo maombi ya Kada za Afya yalikuwa ni 48,705 na Kada ya Ualimu ni 123,211.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliunda Timu Maalumu ya Uchambuzi ambayo ilifanya kazi ya kuchambua na kuhakiki maombi mbalimbali ya ajira. Uhakiki wa maombi umefanyika katika hatua mbalimbali. Kutokana na idadi ya waombaji kuwa kubwa, Timu ya Uchambuzi wa Maombi ya Ajira ilipewa vigezo vya kuzingatia katika mchakato mzima wa uchaguzi wa waombaji ajira kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa haki na uwazi katika zoezi hili. Vigezo vilivyotumika ni kama ifuatavyo:
 
Mwaka wa kuhitimu
Mwaka wa Kuhitimu kilikuwa ndicho kigezo kikuu cha msingi kilichozingatiwa. Katika kigezo hiki, kipaumbele kimetolewa kwa waombaji wenye sifa waliotangulia kuhitimu kwa mfuatano wa mwaka kulingana na hitaji la kada/kozi au kiwango cha Elimu.
 
Umri wa kuzaliwa
Kigezo cha Umri wa kuzaliwa kilitumika kuwapa kipaumbele waombaji wenye umri mkubwa zaidi ya wenzao pale ambapo waombaji walihitimu mwaka unaofanana, na kwamba nafasi zilikuwa chache kwa mwaka husika kuliko idadi ya waombaji. Lengo ni kuwawezesha waombaji wenye umri unaokaribia miaka 45 kuingia katika utumishi wa umma kwa masharti ya kudumu kwa mujibu wa taratibu za ajira zilizopo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top