Ukaguzi wa dawa unaofanywa na mamlaka ya vifaa Tiba na Dawa(TMDA) umeelezwa kuwa na manufaa kwa watumiaji hivyo mamlaka hiyo imeiomba jamii kuiunga mkono.
Hayo yameelezwa Juni 06, 2023 na Mkaguzi wa Dawa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kanda ya Nyanda za juu Kusini Bi Grace Kapande wakati akitoa elimu ya matumizi ya dawa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe
Bi. Kapande ametumia nafasi hiyo kuieleza jamii kupitia wanafunzi hao kwamba kutokumaliza dozi ya dawa mgonjwa anayopewa na daktari inachangia usugu wa dawa
Tumezungumza na Gloria Haule, Magdalena Yona na Amani Elias wanafunzi wa shule hiyo ambao wamepatiwa elimu hiyo na kusema elimu hiyo wataifanyia kazi na kwenda kuifikisha kwa watu wengine
Mamlaka hiyo ya dawa na vifaa tiba ipo wilayani Makete mkoani Njombe ikiendelea kutoa elimu ya matumizi ya dawa kwa makundi mbalimbali kwa lengo la kuielemisha jamii ili iondokane na matumizi holela ya dawa.