Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watanzania kwenda kuanza utekelezaji wa miradi mikubwa ya liganga na mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe baada ya kuanza ulipaji fidia kwa wananchi.
Akizungumza kwa njia ya simu na mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka wakati wa uzinduzi wa zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yenye madini hayo Rais Samia amesema ni lazima wananchi wote walipwe fidia pamoja na kushughulikia changamoto zote ili miradi hiyo mikubwa ianze.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la maendeleo la taifa NDC Dkt Nicolaus Shombe amesema Hadi Jana usiku Watu 39 walikuwa wameshalipwa fedha zao za fidia waliopisha maeneo ya uwekezaji wa madini ya Chuma na Makaa ya mawe Wilayani Ludewa mkoani Njombe na zoezi linaendelea.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga anasema licha ya wananchi wake kuanza kulipwa fidia Lakini bado wanatamani kusikia miradi ya madini hayo inaanza lini kwani wawekezaji wadogo wa mkoa wa Njombe nao wanataka vitalu vya madini.