Watano waliotuhumiwa kumbaka mwanachuo wakamatwa!

0

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewatia mbaroni watu watano wakituhumiwa kuvamia hosteli wanayoishi wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) maeneo ya Semtema, Manispaa ya Iringa, ambapo wanadaiwa kupora na kumbaka mwanafunzi wa chuo hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali walivyokuwa wametumia kunyia uhalifu.

Miongoni mwa vifaa walivyokamatwa navyo ni mapanga matatu pamoja na bajaji yenye namba za usajili MC 206 DFF iliyokuwa ikitumiwa katika uhalifu.

Bukumbi amesema watu wawili kati ya watano waliokamatwa ndio waliotekeleza tukio la ubakaji kwa mwanafunzi wa chuo hicho, na kwa mujibu wa RPC huyo, kitendo hicho kwa mujibu wa sheria kinatambuliwa kama ‘ubakaji wa kundi.’

“Baada ya watuhumiwa kuvunja na kuingia kwenye hosteli walipora kompyuta, simu pamoja na televisheni, baadaye watuhumiwa wawili walimbaka mwanafunzi huyo, kitendo tunachokiita ubakaji wa kundi,” amesema Kamanda Bukumbi.

Wakizungumza Juni 7, 2023 katika Mtaa wa Semtema baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya uhalifu kwa baadhi ya vijana wakiwa na sialaha za jadi kuvamia nyumba na kupora.

Mmoja wa wakazi hao, Agnes Kapinga amesema mwanafunzi aliyefanyiwa ukatili huo anapaswa kusaidiwa kisaikolojia kutokana na tukio hilo.

Kwa upande wao baadhi ya wanachuo waliomba kujengewa hosteli ndani ya vyuo zikiwa na ulinzi tofauti na sasa ambapo wengi wao wamepanga mitaani au kwenye hosteli za watu binafsi zisizo salama.

“Hosteli nyingi zipo huku mitaani na hazina ulinzi wowote, hali hii ni mbaya sana kwani licha ya kuwa na kituo cha Polisi bado hali ya usalama haipo sawa.
Miaka kadhaa iliyopita Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Ritha Kabati alijenga kituo cha Polisi katika eneo la Semtema ili kusogeza ulinzi kwa wanafunzi hao.
credit: Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top