Katika katika ya Umeme yamchefua Msukuma 'BITEKO TUMECHOKA KELELE ZA MAJENERETA'

0

 Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma amemuomba Naibu waziri mkuu na Waziri wa nishati Dotto Biteko kuharakisha upatikanaji wa umeme kwani watanzania wanachoshwa na adha hiyo.

Akizungumza wakati akitoa salamu zake katika ziara ya Naibu waziri mkuu katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita Musukuma amesema wananchi wamechoka kusikiliza kelele za majenereta na kumsihi kuwa waandae mapendekezo kwa Rais ili watanzania waondokane na adha hiyo.

’'Najua sasahivi umepanda mwenzio ndio kwanza nimeanza sasa tunayoshida nchi hii ya kukatika katika kwa umeme ni ‘alarm’ muone ni namna gani mnatutoa kwenye hii katakata ya umeme tumechoka kusikiliza majenereta,mama mzigo anao kaeni mpangilie vizuri mumpelekee proposal mama,watanzania wanataka kusikia tunaachana na mambo ya majenereta ka ka ka kila sehemu hatutaki kusikia hayo mambo’’ Amesema Musukuma

TAZAMA VIDEO YA MSUKUMA HAPA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top