Mwalimu atuhumiwa kumbaka mwanafunzi nyumbani kwake

0

 Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamshikilia mtu mmoja (23) mkazi wa kijiji cha Mkalapa kata ya Chikundi ambaye ni mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Mkalapa kwa tuhuma za kumbaka binti (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo.

 Akizungumza na waandishi wa habari  Septemba 20,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nikodemus Katembo amesema kuwa Septemba 18  katika Kijiji cha Mkalapa, Kata ya Chikundi, Wilaya ya Masasi mkoani wa Mtwara mtuhumiwa huyo alikuwa ni mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Mkalapa.

Amesema kuwa inasemekana kuwa mwalimu huyo alimwita binti huyo nyumbani kwake baada ya kuingia ndani alimkamata na kumziba mdomo ili asipige kelele kisha akaanza kumbaka.

Ambapo mzazi wa binti huyo alipata taarifa za siri kuwa mwanaye ameingia ambapo alibainika kuingiliwa na hali yake ya kiafya inaendelea vizuri ambapo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Nitoe rai kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Pili kukomesha kabisha vitendo hivi vya ukatili dhidi ya watoto.

Aidha jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kuhakiksha kuwa Mkoa wa Mtwara unaendelea kuwa salama.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top