Mgogoro kati ya wafugaji na wakulima katika Kijiji cha Lembapuli, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara umechukua sura mpya baada ya wakulima kudaiwa kuvamia makazi ya wafugaji na kushambulia mifugo kwa risasi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya waathirika wa tukio hilo wamedai lilifanyika usiku wa kuamkia juzi. Watu wanaodaiwa wakulima walivamia makazi na kushambulia mifugo kwa risasi.
Mmoja wa waathirika wa tukio hilo, Sanyakwa Kapande, alidai kuwa watu hao walivamia nyumba yake kisha kuvunja milango na kuvamia zizi la ng'ombe. Baadaye walishambulia kwa risasi ng'ombe kadhaa.
"Wengine waliingia katika zizi la ng'ombe wakaenda kupiga risasi ng'ombe 10. Kati yao, mmoja amekufa wengine wamejeruhiwa vibaya. Siidhani kama watapona kwa sababu wamepigwa risasi tumboni na kuvunjwa miguu," alidai Kapande.
Alipoulizwa chanzo cha tukio hilo, Kapande alidai ni mgogoro wa ardhi kati ya wafugaji na wakulima, ulioibuka tena baada ya kusuluhishwa na mamlaka ya kijiji. soma zaidi>